Wafanyabiashara wa kuuza mazao nje ya nchi kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini wamefanya semina Jijini Arusha iliyoandaliwa na wakala wa usajili wa leseni na biashara Brela nakuwapatia mafunzo ya usajili wa majina ya biashara na kampuni ili kutekeleza miongozo na taratibu za biashara hiyo.
Waziri wa viwanda na biashara Dkt. Ashatu Kijaji alielekeza BRELA kutoa elimu ya usajili wa majina ya biashara na kampuni baada ya kuibuka sintofahamu kwa wafanyabiashara wanaosafirisha mazao nje ya nchi kupitia mpaka wa Namanga.
Mkuu wa kitengo cha usajili wa kampuni BRELA Isdori Nkimi akiwa katika semina ya wafanyabiashara hao amewataka wafanyabiashara kuhudhuria mafunzo hayo yatakayo fanyika kwa siku tatu huku wakiwa na lengo ya kumpunguzia gharama mfanya biashara kwa kurahisisha Huduma na kutoa leseni za Usafirishaji.
Agnes Mushi na Mau Peter ni Wafanyabiashara wa mazao nje ya nchi wameeleza namna elimu hiyo itakavyowasaidia kusajili biashara zao ili wafanye shughuli zao kihalali na itapunguza changamoto walizokuwa wakikutana nazo awali.