Duniani

Baada ya Marekani na Cuba kufungua Balozi zao, zinafuatia safari za ndege…

on

Flight Nice

Cuba walifungua Ubalozi wao ndani ya Washington  Marekani July 20 2015, Marekani nao wamefungua Ubalozi wao ndani ya Havana Cuba August 14 2015, haya matukio yameandika Historia kubwa sana Duniani kwa sababu kwa zaidi ya miaka 50 Mataifa hayo mawili hayakuwa kwenye uhusiano mzuri.

Usafiri muhimu ambao ni kiungo cha kutegemewa kabisa kati ya Marekani na Cuba ni usafiri wa ndege, good news kwa wasafiri toka  Los Angeles kwenda Havana ni kwamba Shirika la Ndege la American Airlines liko kwenye mipango ya kuanzisha safari kati ya Majiji hayo mawili mwezi December 2015.

Hili litakuwa Shirika la pili kuanzisha safari kati ya nchi hizo mbili, Shirika la kwanza ilikuwa ni JetBlue ambao walianzisha safari zao kati ya New York na Havana mwezi July 2015.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments