Akaunti za mashahidi na uchanganuzi wa vipande vya video na silaha zinaonyesha kuwa kombora la Ukrain ambalo lilishindwa kulenga shabaha yake ndilo lililosababisha shambulio baya katika soko la Ukraine mnamo Septemba, gazeti la New York Times liliripoti Jumatatu.
Shambulio la makombora katika soko la Kostiantynivka liliua takriban raia 16 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 30 na hapo awali lililaumiwa kwa Urusi.
Rais Volodymyr Zelenskyy alisema ni “shambulio la kigaidi la makusudi,” kufuatia visa vingine vingi vya mashambulio ya Urusi kwenye miundombinu ya raia. Urusi inakanusha kuwalenga raia.
Hata hivyo, ushahidi uliokusanywa na kuchambuliwa na gazeti la The New York Times – ikiwa ni pamoja na vipande vya makombora, picha za satelaiti, akaunti za mashahidi na machapisho kwenye mitandao ya kijamii “zinadokeza kwa nguvu kwamba shambulio hilo baya lilikuwa ni matokeo ya kombora la ulinzi wa anga la Ukraine lililorushwa na mfumo wa kurusha Buk,” gazeti hilo lilisema katika ripoti iliyochapishwa Jumatatu.
“Shambulio hilo linaonekana kuwa ajali mbaya ,wataalamu wa ulinzi wa anga wanasema makombora kama yale yaliyopiga sokoni yanaweza kupotea kwa sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na hitilafu ya kielektroniki au fini ya mwongozo ambayo imeharibika au kukatwa wakati wa kurusha,” gazeti hilo lilisema.
Uwezekano wa kushindwa kwa kombora kulitokea katikati ya mapigano ya nyuma na mbele yaliyozoeleka katika eneo jirani, gazeti hilo liliongeza, huku vikosi vya Urusi vikiwa vimeshambulia Kostiantynivka usiku uliopita.