Michezo

Ushindi wa Simba kwa TP Mazembe, umebeba dhamana kesi za Wajane 10 (+video)

on

Mchezo wa robo fainali ya CAF Champions League kati ya Simba SC dhidi ya TP Mazembe siku ya Jumamosi ya April 6 2019 umebeba dhamana ya Wajane 10 ambao watasaidiwa bure kesi zao.

Hatua hiyo inatokana na Wakili wa Kujitegemea, Leornad Manyama kusema kuwa endapo Simba SC ikishinda basi atajitolea kusimamia kesi 10 bure za Wanawake Wajane kama zawadi kwa timu yake ye Simba.

Kwa pamoja tuungane kwani mafanikio ya Simba ni mafanikio ya taifa letu, nawaomba wachezaji wakajitume nikiwa kama mwanasheria endapo Simba ikishinda najitolea kusimamia kesi 10 bure kwa wajane wowote wanaonyanyaswa na kunyimwa mirathi yao,”amesema.

Hujafa hujaumbika: Joyce ni Mwalimu anaefundishia kitandani kwa miaka 20

Soma na hizi

Tupia Comments