Michezo

Makampuni yatakiwa kushiriki kukuza mchezo wa golf nchini

on

July 2,2021 Mashindano ya Corporate Masters Golf competition 2021 yazinduliwa rasmi katika Viwanja vya Gymkhana Club DSM na kushirikisha Makampuni mbalimbali.

Waandaji wametoa wito kwa wadau na wapenzi wa mchezo wa golf kutoka Makampuni na Mashirika mbalimbali kujitokeza kushiriki kilele cha Corporate Masters Golf Competition 2021 tarehe 7 mwezi wa nane.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Corporate Masters Golf Competition, Kelly Kairuki amesema “mashindano haya yanatoa fursa kwa wafanyakazi wa makampuni ya kibiashara na wafanyabiashara kukutana na kubadilishana mawazo kuhusu biashara, uchumi huku wakicheza mchezo wa golf”.

Akizungumza kwa upande wa Serikali, Afisa Maendeleo ya Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Milinde Mahona akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Hassan Abbas, ametoa wito kwa Makampuni ya biashara na taasisi mbalimbali kujitokeza kushiriki katika mashindano hayo ili kukuza wigo wa mchezo wa golf nchini na vilevile kupata nafasi ya kubadilishana mawazo ya kibiashara yatakayoweza kuchangia ukuaji wa uchumi nchini pamoja na uwekezaji kwenye sekta ya michezo

Kilele cha mashindano hayo yatafanyika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.

 

 

Soma na hizi

Tupia Comments