Kiungo wa Arsenal raia wa Uruguay, Lucas Torreira, ambaye yuko kwa mkopo Atletico Madrid ya Hispania amesema anataka kuondoka barani ulaya ili aende kukipiga Boca Juniors ya nchini Argentina.
Torreira (25) amesema amefikia kufanya maamuzi hayo baada ya mama yake kupoteza maisha na ugonjwa wa Covid-19 mapema wiki hii.
“Usiku ambao mama yangu alifariki dunia, nilimwambia mwakilishi wangu kuwa sitaki kucheza Ulaya tena na ninataka kuhamia Boca” amebainisha Torreira.