Watu ambao wanapata usingizi wa kupindukia wakati wa mchana au kukosa usingizi kabisa nyakati za usiku wako katika hatari kubwa ya kupatwa na matatizo ya shida ya afya ya akili inayoitwa Motoric Cognitive Risk Syndrome (MCR).
Kulingana na utafiti mpya uliochapishwa katika Jarida la Neurology kutoka Kituo cha Matibabu cha American Academy of Neurology umesema kulala mchana kupita kiasi kunaweza kuongeza hatari ya utambuzi na kusababisha shida ya afya ya akili.
Ingawa utafiti huo haukutaja umri mahsusi, tafiti zinaonyesha kwamba matatizo ya usingizi kwa Watu wenye umri wa miaka 40 hadi 50 yanaweza kuwa viashiria vya mapema au sababu za hatari za kupungua kwa utambuzi katika miaka ya baadaye.
“Iwapo tatizo la kupata usingizi wa mchana au kukosa usingizi hutokea katika umri wa makamo ni muhimu kwa Watu kutafuta matibabu mapema.” Dkt. Verna Porter, Mtaalam wa Neurology kutoka Kituo cha Afya cha Providence Saint John amesema.