Kundi la muqawama wa Palestina Hamas limesema makubaliano yoyote ya kusitisha mapigano Gaza lazima yahusishe kuondolewa kabisa kwa wanajeshi wavamizi wa Israel katika ardhi ya Palestina.
“Makubaliano yoyote lazima yafikie usitishaji vita wa kina, kujiondoa kabisa (Waisraeli) kutoka Gaza, (na) kurejea kwa waliokimbia makazi yao,” afisa wa Hamas Hossam Badran alisema katika taarifa yake baada ya mazungumzo ya kusitisha mapigano kuanza tena huko Doha.
Marekani, Qatar na Misri zilikutana na wajumbe wa Israel nchini Qatar huku idadi ya vifo vya Wapalestina kutokana na vita vya miezi 10 vya Israel ikizidi 40,000.