Mix

UTAFITI: Pombe kwa wanawake kabla ya ujauzito husababisha kisukari kwa watoto

on

Wanasayensi wa Marekani wamesema unywaji pombe kwa wanawake hata kabla ya wazo la kupata watoto unaweza kupelekea kujifungua watoto wenye kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu na mabadiliko mengine kwenye utendaji wa glucose.

Watafiti wa Chuo Kikuu cha Rutgers walifanya utafiti huo kwa panya ambaye utendaji kazi wa glucose unafanana na binadamu ambapo kwa wiki nne waliwapa diet iliyochanganywa na kilevi 6.7% na baadaye iliondolewa na wiki tatu baadaye walizaa.

Watoto wa panya hao walilinganishwa na watoto wa panya ambao hawakuwekewa kilevi kwenye diet kabla ya wazo la kuwa na watoto ambapo watafiti waligundua dalili kadhaa ambazo hazikuwa za kawaida katika utendaji wa glucose.

Mwandishi-mwenza wa utafiti huo Ali Al-Yasari alisema: “Matokeo haya yanaonesha athari za matumizi mabaya ya kilevi kwa mama kabla ya wazo la kupata mtoto ambazo zinaweza kumuathiri mtoto. Mabadiliko haya yanaweza kuwa athari za muda mrefu katika mfumo wa glucose wa mtoto na uwezekano wa kuongezeka hatari ya kisukari.”

Soma na hizi

Tupia Comments