social network

Utani mwingine unaohusu Shilingi yetu ya Tanzania….

on

Kumekua na utani wa aina nyingi sana kwenye mitandao yetu ya kijamii na wewe kama ni mmoja wa watumiaji  utakua unakubaliana na mimi,utani ambao nimekutana nao na umenifurahisha ni huu ambao unaonyesha matumizi ya shilingi mia moja ya Kitanzania toka mwaka 1962 mpaka mwaka huu 2016.

Kwenye hiyo miaka inaonyesha thamani ya pesa hiyo toka mwaka 1962 ambapo mwaka huo 1962 ilikua na uwezo wa kununulia Eka moja ya ardhi,1970 ilikua na uwezo wa kununua nguo za ndoto yako,1990 kununua mche wa sabuni halafu mwaka 2000 ilikua inanunua pakiti za viberiti,waliponichekesha zaidi ni mwaka 2016 eti matumizi yake ni kukwangulia vocha.

WhatsApp-Image-20160703Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Tupia Comments