Nchini Mali, shirika lisilo la kiserikali la Action Against Hunger linabainisha ongezeko la kutisha la visa vya utapiamlo wa watoto katika ripoti iliyochapishwa siku ya Jumanne Agosti 20.
Watoto walio na umri wa chini ya miaka 5 wanaoishi ndani ya kambi za wakimbizi kaskazini-mashariki mwa nchi wameathirika zaidi.
Utapiamlo huathiri asilimia 30 ya watoto katika baadhi ya maeneo. Miongoni mwa sababu za utapiamlo huu wa watoto, shirika hili liataja migogoro mbalimbali nchini Mali inayoendelea tangu mwaka 2012.
Nchini Mali, ongezeko la utapiamlo miongoni mwa watoto linaweza kuelezewa kwa kiasi fulani kutokana na migogoro mbalimbali ambayo imetokea nchini Mali tangu mwaka 2012.
Haya yamewalazimu watu kukimbia, na kuacha majukumu yao yote ya kujikimu, hali inayozidi kuwa mbaya, kulingana na shirika la kimataifa la Action Against Hunger (ACF) katika ripoti iliyochapishwa siku ya Jumanne Agosti 20.
Kulingana na Mamadou Diop, mkurugenzi wa nchi wa Action Against Hunger nchini Mali, “tumefikia viwango vya utapiamlo ambavyo havijawahi kuwa sawa katika miaka 10 iliyopita, vya 30% ya utapiamlo mkali duniani. Na kiwango kikubwa cha utapiamlo cha 11%, ikifahamika kwamba kizingiti cha tahadhari ni 2% kwa utapiamlo mkali.