Michezo

Utata kuhusu umri wa mchezaji huyu wa Lazio wamalizika – haya ndio matokeo ya uchunguzi wa umri wake

on

Sakata la kiungo wa klabu ya Lazio  Joseph Minala aliyetengeneza vichwa vya habari kuhusu umri wake halisi leo hii limepata ufumbuzi.

Mchezaji huyo ambaye taswira yake inaonyesha ni mtu mzima tofauti na umri anaosema kuwa nao mwenyewe – miaka 17, leo imetoka ripoti rasmi inayoonyesha ni kweli na umri wa miaka 17 tofauti na watu walivyokuwa wakisema kwamba ni mtu mzima wa miaka 42.

Kwa mujibu wa chama cha soka cha Italia ni kwamba baada ya uchunguzi wa kina uliofanyika kuhusiana na umri wa mchezaji huyo, imefahamika kwamba ni kweli Joseph Minala ni mtoto wa miaka 17.

Mtandao mmoja wa kiafrika mwezi uliopita uliripoti kwamba Minala amedanganya kuhusu umri wake wa miaka 17, lakini mwenyewe alijitetea kwamba taswira yake ya kiutu uzima inatokana na mazingira magumu aliyokulia nchini kwao Cameroon, hata hivyo ikabidi ufanyike uchunguzi wa kina ili kufahamu ukweli ulivyo.

Matokeo ya uchunguzi huo yametolewa leo na imefahamika kwamba Minala hakudanganya umri na sasa ameruhusiwa kuendelea kuichezea timu ya watoto ya Lazio ya Italia.

 

Tupia Comments