Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke Mhe.Abdallah Mtinika amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Elihuruma Mabelya kufikisha ujumbe kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kuwa baraza la madiwani la Halmashauri hiyo ambalo ndicho chombo cha uwakilishi cha wananchi kuwa wanalihitaji eneo la Temeke mwisho.