Wiki chache tu baada ya msanii Beyonce kuwa msanii aliyepewa tuzo nyingi zaidi katika historia ya Grammys, utawala wa wake bado uliendelea kwenye Tuzo za 54 za kila mwaka za NAACP image awards, ambapo aliongeza tuzo tatu zaidi .
Wakati wa tafrija ya mtandaoni siku ya Jumatatu usiku, Queen Bey alitajwa kuwa msanii bora wa kike wa mwaka huu, huku rekodi yake ya “Renaissance” ilishinda albamu bora na “Cuff It” ilitwaa tuzo ya wimbo bora wa soul/R&B.
Beyoncé alikuwa amefungana na Kendrick Lamar kwa kuchaguliwa mara nyingi zaidi, Wasanii wote wawili walikuwa nominated katika kitengo bora cha video za muziki pamoja na albamu zilizo tazamwa zaidi, lakini kombe lilimwendea Rihanna kwa wimbo wake wa “Black Panther: Wakanda Forever”, “Lift Me Up.”
Filamu ya Marvel pia ilitunukiwa tuzo bora zaidi ya wimbo/mkusanyiko wa albamu.
Beyoncé alikuwa nominated tena katika category ya kikundi bora cha watu wawili, au kushirikishwa, lakini tuzo hiyo ilienda kwa “Call Me Every Day” kutoka kwa Chris Brown feat. Wizkid, lakini ChrisBrown pia alitwaa tuzo ya msanii bora wa kiume kwa albamu yake inayokwenda kwa Mina la ‘’Breezy”.
Beyoncé sasa ana Tuzo 25 za Picha za NAACP katika kipindi chote cha kazi yake, ikiwa ni pamoja na ushindi wa mtumbuizaji wa mwaka 2004 na 2019.
Mwaka huu unakuwa ushindi wake wa nne kwa msanii bora wa kike, baada ya kutwaa taji hilo mwaka wa 2015, 2017 na 2021, “Renaissance” ni rekodi yake ya nne kushinda katika kitengo bora cha albamu – kufuatia wimbo wa “Dreamgirls” (2007), “Lemonade” (2017) na “Homecoming: The Live Album” (2020) – na “Cuff It” Pia ana Tuzo tano za Picha za NAACP kwa kushirikishwa au kikundi bora na Destiny’s Child.