Top Stories

Uteuzi aliofanya Rais Samia leo December 11, 2021

on

Rais Samia Suluhu Hassa amemteua Balozi Ali Siwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Uteuzi huo umefanyika leo Jumamosi Desemba 11, 2021 ambapo Balozi Siwa ameteuliwa kwa kipindi cha pili kushika nafasi hiyo baada ya muda wa bosi hiyo kuisha Septemba 21 mwaka huu.

Aidha Rais Samia pia amewapangia vituo vya kazi mabalozi wanne.

Balozi Said Mussa amekuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait, Balozi Fredrick Kibuta amekuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Balozi Said Mshana amekuwa Balozi wa Tanzania Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo huku Balozi Alex Kalua akipangiwa kuwa Balozi wa Tanzania katika Taifa la Israel.

VITUKO VYA SHABIKI WA YANGA FULL MBWEMBWE APIGA GWANDA ZA KIJESHI NA BUNDUKI

Soma na hizi

Tupia Comments