Mbunge wa viti maalum CCM Kiteto Koshuma amezungumzia madhara yatokanayo na ndoa za utotoni huku akiomba sheria zibadilishwe kutoa adhabu kwa watuhumiwa haya yakiwa ni matokeo ya jitihada zinazofanywa Na mtandao wa kupinga ndoa za utotoni Tanzania (TECMN)
Ambapo wamekuwa wakihusisha wabunge,wazee wa mila,dini na wahanga wa Ndoa za utotoni katika kuhamasisha muswada wa Sheria ya ndoa kuletwa bungeni.
Koshuma amesema…>>>’Watoto wengi wanapoolewa chini ya miaka 15 kiafya wanakuwa hawajapevuka na hizi tunaziita ni mimba za utotoni na madhara yake ni vifo vya wakinamama‘
‘Juzi kuna dada anaitwa Rebeca Gyumi alipeleka mapendekezo yake mahakamani kuhusiana na kubadilisha sheria hii ya ndoa na mahakama ilitoa mapendekezo kwa serikali kubadilisha sheria ya ndoa inayosema kwa mtoto wa kike anatakiwa akiwa na miaka 15 na wakiume kuwa na miaka 18’
Full video nimekuwekea hapa chini tayari…
VIDEO: Alichokiongea Halima Mdee baada ya kukiri kumtukana Spika
BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo