Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameangaza nyongeza ya asilimia 45 ya mshahara kwa wafanyikazi wa umma 700,000 siku tano kabla ya uchaguzi mkuu.
Haya yanajiri wakati uchumi wa nchi hiyo ukiyumba kutokana na athari za matetemeko makubwa ya ardhi mwezi Februari.
Erdogan, ambaye alichaguliwa kuwa rais wa Uturuki mwaka 2014, atawania muhula mwingine katika uchaguzi wa rais na wabunge mnamo Mei 14.
Kura za maoni zinaonyesha Erdogan anakabiliwa na kinyang’anyiro kikali kutoka mgombea urais wa upinzani, Kemal Kilicdaroglu.
Uchumi wa Uturuki ni suala muhimu kuelekea uchaguzi wa Jumapili.
Hatua ya Erdogan ya kupunguza kwa viwango vya riba kusiko kwa kawaida kulisababisha kushuka kwa thamani ya lira ya Uturuki mwishoni mwa 2021 na kufanya mfumuko wa bei kufikia asilimia 85.5 mwaka jana, kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa ndani ya miaka 24.