Habari za Mastaa

Hoteli yajipanga kumuomba radhi Meek Mill

on

Baada ya siku chache rapper Meek Mill kuilalamikia hoteli ya Cosmopolitan kwa ubaguzi wa rangi, leo May 31,2019 imeripotiwa kuwa hoteli hiyo imepanga kuomba radhi hadharani kwa kitendo hicho ambacho kilitokea Jumapili ya May 26.

Meek Mill alitoa malalamiko kuwa alizuiliwa kuingia kwenye hoteli hiyo iliyopo mjini Las Vegas ambapo walinzi wa eneo hilo walisema kuwa hakufata utaratibu uliowekwa kwenye hoteli hiyo na endapo ataingia lazima wamkamate. Ilielezwa kuwa rapper huyo alikwenda kwa nia ya kuhudhuria tamasha la Dj Mustard.

Iliripotiwa kuwa Mwanasheria wa rapper huyo, Joe Tacopina aliandika barua ikiwataka wamiliki wa hotel hiyo kuomba radhi kwa kitendo hicho ikiwa ilielezwa kuwa ni tabia ya hoteli hiyo kuwazuzia mastaa weusi kuingia mahali hapo.

VIDEO: REKODI KUMI ZA ‘KIJINGA’ ZAIDI ZILIZOINGIA KWENYE KITABU CHA “GUINNESS”

Soma na hizi

Tupia Comments