AyoTV

Waziri Mwakyembe katangaza Dreamliner imeshindwa kuipeleka Taifa Stars nchini Cape Verde

on

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars usiku wa leo October 9 2018 itasafiri kuelekea Cape Verde kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu kucheza michuano ya mataifa ya Afrika AFCON 2019 nchini Cameroon, Taifa Stars awali walikuwa wasafiri na ndege ya Air Tanzania Dreamliner lakini imeshindikana.

Waziri wa habari utamaduni sanaa na michezo Dr Harrison Mwakyembe amethibitisha kuwa  Dreamliner haiwezi kwenda na badala yake wamekodi ndege nyingine maalum kwa ajili ya safari hiyo, Dreamliner imeshindwa kwenda kutokana na uwanja wa ndege waliopaswa kutua haiwezi kupokea ndege kubwa kama Dreamliner.

“Simba tumewaachia, sisi hatuna presha”-Kocha wa Yanga

Soma na hizi

Tupia Comments