Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) mkoa wa Iringa umeendesha bonanza kubwa la michezo lililohusisha vijana wa shule za sekondari mkoani humo kwa lengo la kutoa hamasa kwa vijana kuona umuhimu wa kujiandikisha kwenye Daftari la Makazi na hivyo kuwa tayari kushiriki kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 17 2024.
Bonanza hilo lililoandaliwa na UVCCM mkoa wa Iringa pia limedhaminiwa na Kampuni ya maziwa ya ASAS ya mkoani Iringa.
“Leo hii Tarehe 10 sisi kama UVCCM tuliamua kuandaa Bonanza hili kubwa kuwakutanisha vijana wa makundi mbalimbali kama vile wanafunzi, madereva bodaboda na bajaji. Dhumuni kubwa ni kuweza kuwakumbusha vijana kujiandikisha maana zoezi la uandikishaji linaanza 11 Novemba”- Amesema Tonga.
Amesema pia Bonanza hilo limetumika kama jukwaa kwa ajili ya kutoa elimu ya Lishe ili kuijengea uwezo jamii katika kukabiliana na tatizo la udumavu ambalo linaendelea kuisumbua jamii ya watu wa mkoa wa Iringa.
Aidha Tonga amesema jumuiya hiyo imetumia tukio hilo kutoa kuhamasisha elimu ya usalama wa wanafunzi hususani wanafunzi wasichana.