AyoTV

VIDEO: UVCCM wamezungumzia kuhusu sakata la uteuzi wa Jokate

on

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ‘UVCCM’ kupitia Kamati ya Utekelezaji ilifanya uteuzi wa Wakuu wa Idara za Makao Makuu  ambapo Mwanamitindo Jokate Mwegelo ameteuliwa katika Idara Uhamisishaji na Chipukizi.

Baada ya uteuzi huo wa Jokate, ilidaiwa kuleta mtafarano ndani ya umoja huo ambapo baadhi ya wanachama wake wakidai utaratibu uliotumika haukuwa sahihi.

Ayo TV na millardayo.com imefanya juhudi za kumtafuta Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka ambaye ameutolea ufafanuzi uteuzi wa Jokate akisema kuwa hakuna kanuni iliyovunjwa katika uteuzi wa wakuu hao.

“Jiuhakikishie umma wa Tanzania kwamba hakuna kanuni ya Umoja wa Vijana iliyovunjwa katika uteuzi ama kuwakaimisha Wakuu hawa wa Idara.” – Shaka Hamdu Shaka.

Bonyeza play kutazama…

VIDEO: Alichokizungumza Jokate baada ya uteuzi wake UVCCM. Bonyeza play kutazama…

Soma na hizi

Tupia Comments