AyoTV

VIDEO: Alichokizungumza Jokate baada ya uteuzi wake UVCCM

on

Siku chache zilizopita Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ‘UVCCM’ kupitia kwa Kamati ya Utekelezaji ulifanya utezi wa Wakuu wa Idara mbalimbali za Makao Makuu ambapo mmoja wa walioteuliwa ni mwanamitindo Jokate Mwegelo.

Jokate ameteuliwa kuwa Kaimu Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi katika uteuzi ambao ulizua sintofahamu ndani ya Umoja huo ambapo baadhi wakihoji uhalali wa mamlaka iliyomteua.

Ayo TV na millardayo.com imempata Jokate ambaye anaeleza juu ya uteuzi wake ndani ya UVCCM.

“Nimeupokea kama dhamana. Taasisi kubwa iliyoasisiwa takribani miaka 40, wakikuamini wewe katika nafasi yoyote ndani ya Taasisi hiyo, ni dhamana. Na nimepokea kama dhamana na nimepokea kama wao wana imani na mimi naweza nikawa na mchango fulani katika kuendeleza Idara ambayo wamenipatia.” – Jokate Mwegelo.

VIDEO: UVCCM wamezungumzia kuhusu sakata la uteuzi wa Jokate. Bonyeza play kutazama…

Soma na hizi

Tupia Comments