Baraza la Madiwani katika Manispaa ya Geita Mkoani Geita limesikitishwa na Baadhi ya Vitendo vya Uvunjifu wa amani ambavyo vimekuwa vikifanywa na Baadhi ya Vijana wilayani humo huku wakiviomba vyombo vya Usalama kuingilia kati Uharifu unaofanywa na Vijana hao.
Hayo yameelezwa katika kikao cha Baraza la Madiwani wakati wakijadili taarifa ya robo ya Pili ya Mwaka 2024/ 2025 ambapo Baadhi ya Madiwani akiwemo Diwani wa kata ya Bombambili Leonard Bugomola na Zaituni Fundikira Diwani wa Viti Maalumu kata ya Kalangalala wamepaza sauti ya kuwepo kwa vitendo vya wizi , uvutaji Bangi pamoja na wananchi kuporwa Mali zao.
” Vile vikundi vya waharifu ambao wamekwenda kwenye eneo la uwekezaji Bombambili wanaovuta bangi sikanka na vitu vingine ambavyo vinapelekea watoto badala ya kuingia madarasani wanakwenda kukaa na tumesha kuwakurupusha zaidi ya Mara mbili mara tatu sasa ndio maana hii changamoto nimeileta ili tuweze kupatiwa ufumbuzi , ” Diwani kata ya Bombambili , Leonard Bugomola.
Katika hatua nyingine Diwani wa Viti Maalumu kutokea kata ya Kalangalala Bi. Zaituni Fundikira amesema changamoto iliyopo katika Mitaa ya Kalangalala ukiwemo mtaa wa mission ni uwepo wa watoto wanaoishi katika Mazingira magumu ambao wamekuwa kichocheo cha Matendo ya uharifu ikiwemo kuvunja nyumba na kuiba vitu mbalimbali.
” Mh Mwenyekiti hawa watoto wa mtaani tumejitahidi kuwafukuza na tumejitahidi kuwafanyia utaratibu wa kuwarudisha ndio maana wanazaa athari mbaya kwa watoto wetu wengine ambao ni watoto wazuri Mh Mwenyekiti hawa watoto wanatupa athari kubwa kwenye majumba yetu kwa sababu mtaa wetu wa mission wameenda kuiba na wanabomoa wanadumbukiza wale watoto wanaiba lakini walinzi walijitahidi kuwakamata , ” Diwani wa viti maalumu kata ya Kalangalala , Zaituni Fundikira.
Janeth Mobe ni Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Geita katika Baraza hilo amesema tayari Ofisi ya Mkuu wa wilaya kwa kushirikiana na Vyombo vya Usalama wameanza kufanya Doria ya kuwasaka watu hao ambao wamekuwa wakifanya virendo hivyo na kupelekea kuvunja sheria za nchi.
“Ni kweli kuna shida kunaanza kuteteleka suala la usalama pale Bugulula kuja Geita ama kutoka kamwanga kuja Geita changamoto iko kubwa Bodaboda pale tujipange jambo hili sasa linatia shaka ko palikuwa na utulivu lakini sasa naona kam vile wanaona sijui serikali imejisahau wameanza vibaka vibaka pale ikifika jioni wanavizia watu na samaki wanavizia Bodaboda nadhani kama ulivyosema das niwapongeze kwa kuliona hilo , ” Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Geita, Barnabas Mapande.