AyoTV

“Tunakamilisha ulipaji wa fidia kwa ajili ya ujenzi wa Mwendokasi” RC Makonda

on

Leo January 10, 2019 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema serikali inakamilisha mchakato wa ulipaji wa fidia katikati ya jiji la Dar es Salaam kuelekea Mbagala kwa ajili ya ujenzi wa barabara za ‘Mwendokasi’.

Pia amesema kuna miradi kupitia fedha za ufadhiri ambapo serikali inaingia  ubia wa ujenzi wa Fly Over kutokea Agha Khan kuelekea Coco Beach ikiwa ni urefu wa Kilometer 9.6.

“Kasi ni kubwa mno kwani kuna miradi mingine ya barabara, taa na mito pamoja na utengenezaji wa stendi na ule wa Kata 14 ambazo zinaenda kujengwa upya, hivyo tunaendelea na tunafurahishwa na ujenzi huu,”amesema.

Mbali na hilo pia amesema kuna ujenzi wa njia nne kutokea Shekilango hadi Bamaga ambapo tayari suala la uamishaji wa miundombinu umeanza.

TAHADHARI YA WAZIRI JAFO KUHUSU MAJUNGU TAMISEMI “UNAPIGWA DOZI CC 10”

Soma na hizi

Tupia Comments