Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) inatarajia kuanza mpango wa kununua maji kwa kutumia Mita, ambapo hatua ya awali imeshakamilika na hatua ya pili inasubiri kutangazwa kwa zabuni.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Injinia Cyprian Luhemeja amesema mpango huo ulianza na hatua ya awali imeshakamilika japo kumekuwa na changamoto katika teknolojia kutokana na awali kutokuwepo kwa mfumo wa namna hiyo.
Injinia Luhemeja amesema walianza majaribio ya mfumo huo kwa kutumia MITA 10 za awali ambapo wamefanikiwa kwa asilimia kubwa, hivyo wanasubiri hatua ya pili ya kutangaza zabuni kwa ajili kushindana ili uweze kuanza kwa haraka.
Katika hatua nyingine, Injinia Luhemeja amesema mamlaka hiyo inatarajia kuwarudisha maji wateja wake waliokatiwa kutokana na madeni ambapo kwa sasa wataweza kulipa madeni yao kidogo kidogo huku wakiendelea kutumia maji.
WALIOKATIWA MAJI KISA MADENI, DAWASA YATOA MSIMAMO HUU…