Taifa la Morocco kwa sasa linatajwa kuwa moja ya mataifa yenye nguvu kisoka katika bara la Afrika kutokana na kupiga hatua kubwa katika soka siku hadi siku.
Hakuna mashaka hata kidogo moja kati ya watu waliochangia hilo Mfalme wa Morocco Mohammed VI ambaye ndio kiongozi Mkuu wa Taifa hilo.
Ushindi wa 1-0 wa Timu ya Taifa ya Morocco ya Wanawake dhidi ya Colombia katika mchezo wa fainali za Kombe la Dunia la Wanawake linaloendelea nchini Australia limeipa tiketi ya kwenda kucheza 16 bora ya michuano hiyo.
Japokuwa walianza mchezo wao wa kwanza kwa kipigo dhidi ya Ujerumani lakini Morocco wamekata tiketi ya 16 bora na Ujerumani kutolewa kutokana na kumaliza nafasi ya tatu katika kundi H.
Baada ya mafanikio hayo na ukizingatia timu yao ya wanaume katika fainali za Kombe la Dunia za Wanaume 2022 zilizochezwa nchini Qatar na kushuhudi Taifa la Morocco likiandika historia ya kuwa Taifa la kwanza la Afrika kuwahi kufika nusu fainali ya Kombe la Dunia la Wanaume, wananchi wa Taifa hilo wamempongeza Mfalme wa Taifa hilo Mohammed wa VI kwa kuwekeza katika michezo kitu ambacho kimeanza kuzaa matunda.
Mfalme wa Morocco Mohammed VI anaonekana alikuwa na mapenzi na mchezo wa soka toka akiwa mdogo hiyo inatokana na 1976 wakati akiwa na miaka 13 akiwa kama mtoto wa Mfalme (Prince) ambaye alikuwa sehemu ya watu waliopokea Timu yao kwa ushindi wa AFCON 1976.
Uwekezaji wa Mfalme Mohammed wa VI umeongelewa pia na Kocha wao Msaidizi wa Timu ya Taifa ya U-23 Isaam Charai wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari na kutolea mfano uwanja wa Mohammed VI Football Complex ambayo ni moja kati ya kituo na uwanja bora wa kisasa wa kukuza vipaji kama vilivyo vituo vya Clairefontaine cha Ufaransa na St George Park cha England.
Hakuna timu itakuwa na kituo bora kama hicho halafu ikashindwa kufanya vizuri, hiyo ilikuwa Kambi ya Timu ya Taifa ya Morocco.
“Hakuna shaka yoyote kuwa Mfalme Mohamed VI wa Morocco ni moja ya viongozi barani afrika wenye kupenda kuona maendeleo kwenye michezo”
“Tangu Maadhimisho ya siku ya Mfalme jumapili iliyopita Morocco imepiga hatua nyingine katika soka la kimataifa baada ya kuungana na Nigeria na Afrika kusini kutinga 16 Ya kombe la dunia la wanawake”