Habari za Mastaa

Lil Wayne alitaka daftari lake lililopigwa mnada wa zaidi ya Tsh Mil.500

on

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Rapper Lil Wayne atangaza kulihitaji daftari lake lenye ngoma zake kadhaa ambalo lilitangazwa kuuzwa siku kadhaa zilizopita kwa kiasi cha zaidi Milioni 500 za Kitanzania na kampuni ya Moments In Time.

Inaelezwa kuwa kijana mwenye daftari hilo ametoa kauli na kusema kuwa Lil Wayne atatakiwa kununua daftari hilo kama wengine ambavyo wangefanya . Inaripotiwa kuwa wakili wa Weezy ameandika barua ya onyo kwa kampuni ya Moments In Time na kudai kuwa mmiliki wa daftari hilo ana haki na hivyo kijana huyo hana mamlaka ya kukiuza wala kumkabidhi mtu yeyote.

Kikundi cha rapper huyo kimedai kuwa  Wayne hakulitupa dafatri hilo bali alilipoteza na kijana mwenye daftari hilo alilificha kwa miaka mingi na hivyo kwa sasa anaonekana kutafuta hela kupitia daftari hilo ambalo Wayne aliandika mistari kadhaa mwaka 1999.

VIDEO: UTACHEKA!! PIERRE AMPIGIA ALIKIBA LIVE VIDEO CALL AKIMUONESHA

Soma na hizi

Tupia Comments