AyoTV

Rammy kuhusu mahusiano na movie aliyoigiza na Masogange (+Video)

on

Muigizaji staa kutoka Bongomovie, Rammy Galis leo July 14, 2017 amefunguka sababu za kuvunjika kwa mahusiano yake na Agnes Masogange huku akizungumza pia kuhusu movie mpya waliyoitengeneza kabla ya penzi lao kuvunjika.

Ayo TV na millardayo.com zimekutana na Rammy Galis na alianza kwa kusema:>>>”Mahusiano ni mahusiano tu na haikuwa ndoa. Kama ilikuwa mwanzo tukawa pamoja baadaye ikafikia mwisho tukaachana. Hivyo kama mtu ana mapungufu hakuna sababu ya mimi kuendelea naye. Sasa hivi nina mchumba ambaye yuko bara la America na tunajaribu kuyaweka mambo yetu vizuri.

“Mimi kwanza sio mchoyo, jina langu lenyewe ni mtu mwenye ukarimu. Kwa hiyo, kipindi nilipokuwa na Agnes Masogange nimefanya naye vingi ikiwemo tumeigiza movie mpya ambayo imeelezea uhusiano wetu. Kwa hiyo watu wakae tayari kuja kuipokea hiyo movie mpya.” – Rammy Galis

Baada ya Diamond na Alikiba, Mo Music katangaza kuja na biashara hii!!!

Soma na hizi

Tupia Comments