Michezo

Hakika ulikuwa ni usiku wa Mabingwa, Liverpool imeishangaza Barcelona Anfield

on

Moja kati ya michezo mikubwa katika michuano ya UEFA Champions League ya nusu fainali kati ya Liverpool dhidi ya FC Barcelona, mchezo huu unatajwa kuwa mkubwa sababu wa ukubwa wa timu zenyewe na ukitabiriwa kuwa bingwa wa michuano ya UEFA Champions League atatokea katika mchezo huo.

Baada ya FC Barcelona kupata ushindi wa 3-0 katika mchezo wao wa awali katika uwanja wao wa Nou Camp, Barcelona walihitaji sare tu au kupoteza kwa kuanzia magoli 2-0 kushuka chini ili kuingia fainali, kwani Liverpool iliaminika kuwa itaingia katika uwanja wake wa Anfield kuikaribisha Barcelona wakiwa na hofu baada ya kupoteza mchezo wa kwanza.

Liverpool wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani huku wakiwakosa wachezaji wao muhimu kama Mohamed Salah anayesumbuliwa na majeraha ya kichwa na Roberto Firmino, wamefanikiwa kupindua matokeo na kuibuka na ushindi wa magoli 4-0, magoli ambayo yalifungwa na wachezaji wawili ambao walifunga mawili mawili kila mmoja Divock Origi na Wijnaldum, kivuti zaidi ikiwa ni akili ya haraka ya Alexander-Arnold aliyepiga kona iliyokuwa assist ya goli la nne kwa Liverpool na kufungwa na Origi.

Ushindi huo sasa utawafanya Liverpool kuingia fainali ya UEFA Champions League kwa mara ya pili mfululizo lakini hii itakuwa ni mara yao ya tisa katika historia huku wakisubiri kujua mshindani wao katika mchezo wa Tottenham dhidi ya Ajax iliyoshinda 1-0 katika mchezo wa kwanza ugenini, fainali ya michuano hiyo itachezwa katika jiji la Madrid Hispania.

Kigezo kilichoichuja Yanga na kuipa Simba SC nafasi ya kucheza na Sevilla ya Hispania

Soma na hizi

Tupia Comments