Unaweza usiamini lakini kwa mujibu wa utafiti uliyofanywa na BBC, umetaja watu wenye uwezo wa kuona na kutafakari mambo kwa haraka zaidi duniani na Kabila la Himba kutokea Namibia limetajwa kama jamii yenye watu wenye uwezo mkubwa zaidi wa kuona na kukielewa kitu kwa haraka zaidi.
Utafiti huo ulionesha watu wa jamii ya kabila la Himba wana uwezo mkubwa wa kufocus na kuona vitu vidogo ambavyo ni vigumu kuonwa na watu wengine. Kutotumia teknolojia ya aina yoyote kwa watu hao kumetajwa kama sababu kubwa inayochangia watu wa jamii ya Himba kuwa na uwezo mkubwa wa kuona jambo kwa haraka.
Kwa mujibu wa utafiti huo watu wa jamii ya Himba wana uwezo mkubwa wa kuona jambo na kulituma kwa haraka katika ubongo kuliko watu wengine wa kawaida, Ripoti hii ilionesha jinsi gani teknolojia kama simu, Tv na hata computer zinavyoathiri watu wengi na kuchangia kua na uzito na kutafakari mambo kwa haraka.
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO TV MARCH 8 2017? UNAWEZA KUIANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI.