Michezo

Messi kaeleza kinamfanya Van Dijk kuwa mgumu kupitwa na washambuliaji

on

Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina ambaye pia ni nahodha wa timu hiyo na club ya FC Barcelona ya nchini Hispania Lionel Messi, amefunguka katika mahojiano yake na Marca na kueleza kwa nini huwa ni vigumu kumpita beki wa Liverpool Virgil van Dijk na kwenda kufunga.

“Ni beki ambaye anajua timing yake na anasubiri wakati sahihi wa kwenda kuucheza mpira na kumpa changamoto mshambuliaji, yupo fasta na mkubwa lakini ana uwezo mkubwa kwa kimo chake, anavutia pia kwa sababu anajua kulinda na kushambulia na anafunga magoli mengi”>>>> Lionel Messi

Messi alicheza dhidi ya Van Dijk katika mchezo wa nusu fainali ya UEFA Champions League msimu uliopita (2018/2019) na kufunga mara mbili, ila uimara wa Van Dijk uliifanya Liverpool kupata matokeo chanya nyumbani Anfield na kupindua matokeo hadi fainali.

Van Dijk ambaye kwa sasa anatajwa kama beki bora dunia anawania tuzo ya Ballon d’Or Messi na Ronaldo lakini Van Dijk aliwashinda Messi na Ronaldo katika tuzo ya mchezaji bora wa UEFA ila Messi aliwashinda pia wa wawili hao katika kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa FIFA hatujui Ballon d’Or atashinda nani,

AUDIO: SERGIO AGUERO WA MAN CITY AMEPATA AJALI

Soma na hizi

Tupia Comments