Mix

VideoFUPI: Umeipata hii kutoka Ghana ya kukodi watu katika mazishi

on

Inawezekana ikakushangaza kutokana na sehemu au nchi unayotoka isiwe utamaduni wako kuona wakati wa mazishi kuna watu wanacheza wakati wakiwa wamebeba jeneza la marehemu kama sehemu ya shamrashamra za mazishi.

Imeripotiwa na BBC News kuwa Ghana kuna vikundi maalum kwa ajili ya kubeba jeneza yaani mfiwa unakodi watu hao ambao watabeba jeneza kwa shamrashamra na mbwebwe siku ya mazishi kama sehemu ya kusherehekea siku ya mwisho ya marehemu hapa duniani.

Wazo la vikundi vya kukodiwa kwa ajili ya mazishi nchini Ghana unaambiwa limefanikiwa kutoa ajira kwa wanawake na wanaume zaidi ya ajira 100, unaweza tazama video fupi na kuniachia comment yako vipi hii ikija Tanzania inafaa?


ULIKOSA??? Prof. Lipumba afunguka, ajibu tuhuma alizotoa Maalim Seif…tazama hapa!!! 

Soma na hizi

Tupia Comments