Habari za Mastaa

Uzinduzi kipindi kipya cha Salama Jabiri, Ben Pol kazungumza

on

Mtangazaji Salama Jabiri amezindua kipindi chake kipya  ambacho kitakuwa kikiruka East Africa TV na tayari akiwa ameshafanya mahojiano na Mastaa wasiopungua kumi na mbili na wote watakuwa wakionekana kwenye show yake hiyo mpya.

Salama ameleza kipindi hicho kitakuwa tofauti na vipindi vyake vilivyowahi kupita kwani hiki hakitakuwa kiki deal na mastaa tu bali hata watu wa kawaida ilimradi awe na story nzuri itakayo vutia.

Utofauti kati ya kipindi changu kilichopita ni kipindi Kilichokuwa kinafanyika saloon na nilikuwa Sipo peke yangu lakini sahivi Nipo peke yangu na tunajaribu kupata vitu kutoka kwa watu pengine labda vilikuwa havijawahi kutoka before” – Salama Jabiri 

Katika uzinduzi huo Salama alialika watu mbali mbali wakiwemo Mastaa ambapo moja Mastaa hao waliozungumza ni pamoja na msanii Ben Pol ambaye ameelezea utofauti wa show hii ya Salama na Show zake zilizopita akisema hata yeye amefanya Interview ambayo hajawai kufanya sehemu nyingine.

“Nahisi hii show itakuwa kubwa zaidi kwa Sababu iko ki-feature zaidi na zani kupitia hii program watu wanaweza kuwajua vizuri watu wanaowapenda, Mimi nimefanya naye kipindi nadiriki kusema mtu asizani kama anamjua Ben Pol mpaka atakapokitazama hicho kipindi” Msanii BEN POL

Soma na hizi

Tupia Comments