Moja kati ya stori zinazo-trend kwa sasa ni pamoja na hii ya kocha wa zamani wa Dar es Salaam Young Africans ambaye alipandishwa cheo na kuwa Mkurugenzi wa Ufundi, mholanzi Hans van Pluijm, ameripotiwa kufutwa kazi na Yanga habari ambazo hazijathibitishwa na Yanga.
Kwa mujibu wa habari ambazo zimeenea katika mitandao ya kijamii kwa sasa ni kuwa Hans van Pluijm amefutwa kazi na Yanga kwa lengo la kubana matumizi, lakini wengine wanadai kuwa aliongea na moja kati ya magazeti ya Tanzania na kunukuliwa akisema kuwa kama angekuwepo yeye asingefungwa na Simba.
Yanga bado hawajakubali na wala kukanusha kuhusiana na stori hizo za kumfuta kazi Hans, AyoTV ilimpata katibu mkuu wa Yanga Boniface Mkwasa azungumzie tetesi hizo “Kiukweli tamko ramsi kuhusiana na suala hilo litatolewa lakini kwa sasa tunafikiria kusafirisha timu kwenda Morogoro “
ALL GOAL: SIMBA VS YANGA FEBRUARY 25 2017, FULL TIME 2-1