Kuhakikisha hupitwi na stori yoyote ya town millardayo.com leo March 31, 2017 inakusogezea stori kutoka jijini Arusha kwenye VAA Africa Festival Arusha 2017 likiwa ni Tamasha jipya la mitindo ya mavazi Tanzania ambalo limeanzishwa kwa lengo la kuinua wajasiriamali wabunifu.
Kupitia maoneesho hayo wabunifu wanaweza kutangaza kazi zao na kupata nafasi ya kukutana na watu mbalimbali waliofanya vizuri kwenye soko la ubunifu ndani na nje ya Tanzania. Tamasha hilo limeanzishwa mwaka huu ambapo litakuwa linafanyika mara tatu kwa mwaka katika mikoa ya Arusha, Mwanza na Dar es Salaam.
Video: Kilichosababisha Meneja wa Diamond Platnumz, Babutale ailalamikie sekta ya Utalii TZ.>>>