Top Stories

Gari ya FFU imepinduka kutokana na mwendokasi imeua askari 2, Kamanda Mpinga ameongea

on

January 19, 2018 Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya Mohammed Mpinga amezungumza na waandishi wa habari na kutoa taarifa juu tukio la ajali ya barabarani lililotokea January 18, katika barabara kuu ya Mbeya kwenda Tunduma.

Kamanda Mpinga amesema  gari yenye namba za usajili PT 2079 Toyota Land Rover ambayo ni mali ya Jeshi la Polisi Kikosi cha FFU – Mbeya  ilikuwa inaendeshwa na askari  PC Adam iliacha njia na kupinduka na kusababisha vifo kwa askari wawili ambao ni Mathew Jailos Mpogole,26, na  Prosper Jordan Chalamila,29.

Katika ajali hiyo, askari 9 wamejeruhiwa ambapo kati yao wawili wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya na majeruhi saba wametibiwa na kuruhusiwa.

Kamanda Mpinga ametaja chanzo cha ajali hiyo kuwa mwendokasi wa dereva akijaribu kuyapita magari mengine pamoja na utelezi katika barabara na bado upelelezi unaendelea.

MAAMUZI YA SERIKALI YA TZ KUHUSU MELI ZILIZOKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA NA SILAHA

Soma na hizi

Tupia Comments