Michezo

Van Gaal amzungumzia Ramos, na pia amedokeza juu ya usajili wa mshambuliaji mpya Man Utd

on

Zikiwa zimebaki wiki takribani wiki 5 kabla ya dirisha la usajili barani ulaya halijafungwa, kocha wa Manchester United – Louis van Gaal amesema kwamba klabu yake ipo sokoni kutafuta mshambuliaji wa kumsajili kabla muda wa usajili haujaisha – huku akisisitiza mchezaji anayemtaka bado hajaandikwa na vyombo vya habari.

  Katika hatua nyingine boss huyo wa Manchester United aliulizwa juu ya tetesi za usajili wa beki Sergio Ramos wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari, akasema: “Siwezi kuzungumzia tetesi. Nimeshasema kwamba usajili ni mpango endelevu na labda Mr Ramos yupo katika mpango wetu huo, huwezi kujua,” alisema kocha huyo wa kidachi.

Van Gaal pia amethibitisha kwamba golikipa David de Gea ataukosa mchezo wa pili wa majaribio wa United huko Marekani kutokana na majeruhi yanayomsumbua.

Tupia Comments