Michezo

Kauli ya Louis van Gaal kwa kiongozi anayelaumiwa kumkosa Pedro ipo hapa

on

Klabu ya Manchester United ya Uingereza bado haiamini kilichotokea kwa kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho kumbadili uelekeo Pedro Rodriguez kutokea FC Barcelona kwenda katika klabu ya Chelsea na sio Manchester United kama ilivyokuwa awali.

741a48208dbefd0c4cf8443acc831484

Baada ya mpango wa kumpata Pedro kuyeyuka mashabiki na wapenzi wengi wa Man United wamekuwa wakipeleka lawama nyingi kwa makamu mwenyekiti wa Man United Ed Woodward kwa kushindwa kukamilisha mpango huo mapema kwani FC Barcelona na Man United walikuwa washakubaliana kuuziana nyota huyo.

Louis van Gaal

Simu moja pekee ilyotoka kwa Jose Mourinho kwenda kwa Pedro ilitosha kumfanya mshambuliaji huyo kubadili uelekeo wa kwenda na lawama zote kwenda kwa Ed Woodward kuwa  ni mzembe kwani FC Barcelona walishakubali dau la pound milioni 21 ili kumuachia Pedro.

Sasa August 21 kocha wa klabu ya Man United Louis van Gaal amemkingia kifua makamu mwenyekiti wake kwa lawama anazotolewa na wapenzi na mashabiki wa klabu hiyo ila kwa upande wa Van Gaal bado anaimani na Ed Woodward.

Mourinho-Pedro-Chelsea-Conmigo-importante_MDSVID20150713_0114_17

“Nafikiri mnataka kututenganisha na Ed Woodward kamwe haiwezekani kwa sababu kila siku nimekuwa nikipokea vitu vipya kutoka kwake na namuamini sana sifikiri kama tunatakiwa kuwa na mashaka na Ed Woodward kwani amesha tuthibitishia kwa wachezaji wengi kwa miaka mingi amekuwa mtu sahii katika tukio sahii”>>> Louis van Gaal

Ed Woodward alisafiri jumatatu ya August 17 na kuelekea FC Barcelona kumaliza mpango wa kumsajili Pedro kwa ada ya uhamisho ya pound milioni 21.4 kabla siku tatu baadae kutangazwa kusajiliwa na mabingwa wa Ligi kuu Uingereza Chelsea.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments