Michezo

Mfanyakazi aliesimamishwa kazi baada ya kupiga hii picha na Van Persie kwa kina Rihanna.

on

Robert-Van-Persie-and-the-hotel-worker-Kyson-FordeHii imetokea Barbados kwenye nchi alikozaliwa Rihanna ambako muhudumu wa Mgahawa wa Cliff aitwae Kyson Forde amesimamishwa kazi baada ya kupiga picha ya na mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Robin van Persie.

Kilichosababisha uamuzi huo kwa Kyson ni katazo la mgahawa huo kwa wafanyakazi wake kutotumia simu za mkononi kwenye sehemu ya kulia chakula.

Chanzo cha habari kinaeleza kwamba RVP akiwa na familia yake kwenye mgahawa huo, alifuatwa na Keyson ambaye ni shabiki mkubwa wa Manchester Utd na kuombwa kupiga nae picha ambapo alifanikiwa na kisha akaitundika kwenye mitandao ya kijamii ambako kulipelekea boss kuiona na kumsimamisha kazi.

Screen Shot 2014-07-28 at 3.15.31 AM

Van Persie na familia yake mapumzikoni Barbados

Van Persie yupo Barbados mapumzikoni baada ya kuiongoza timu yake ya taifa Uholanzi kushika nafasi ya 3 kwenye kombe la dunia nchini Brazil 2014.

Ni halali yako kupata kila kinachonifikia mtu wangu na niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza hapa >>> twitter Insta FB

Tupia Comments