Ad
Ad

Michezo

Mc Donaldo Mariga ameanza kampeni za Ubunge Kenya

on

Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars ambaye amewahi kuichezea club ya Inter Milan na Parma za Italia McDonald Mariga ameanza kampeni zake za kuwania kiti cha Ubunge wa jimbo la Kibra nchini Kenya kupitia chama cha siasa cha Jubilee.

Baada ya Mariga kustaafu kucheza soka sasa ameamua kuelekeza nguvu zake katika siasa na sasa anawania kiti cha Ubunge, Mariga ameanza kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo hilo kuelekea uchaguzi utakaofanyika November 7 2019, baada ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo kufariki.

Kama hufahamu Mariga katika upande wa soka anabakiwa kuwa mchezaji pekee raia wa Afrika Mashariki aliyewahi kushinda taji la UEFA Champions League (2010) akiwa na Inter Milan chini ya Jose Mourinho, hata hivyo Mariga amepata nafasi ya kugombea jimbo hilo baada ya kuwashinda wagombea wengine 16 katika kura za maoni.

EXCLUSIVE: SAMATTA KAFUNGUKA DILI LAKE KWENDA ENGLAND, VIPI CHAMPIONS LEAGUE

Soma na hizi

Tupia Comments