Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Young Thug atangaza kugombea Urais Marekani

on

Mkali wa Hip Hop kutokea nchini Marekani anayetamba na ngoma ya ‘The London’ Young Thug ametangaza nia ya kugombea Urais nchini humo ifikapo mwaka 2024 na huku akimtaja msanii mwenzake Gunna kama Makamu wa Rais.

Mkali huyo wa rap ameitangaza nia ya kuja kuwa Rais kupitia ukurasa wake twitter ambapo aliandika “Nitagombea Urais 2024, Gunna atakuwa makamu wa Rais” . Young Thug ni baba mwenye watoto 6 hata hivyo jamii inayomzunguka imedai kuwa rapper huyo ana upendo mkubwa kwa watoto kauli hii imethibitishwa siku kadhaa zilizopita baada ya Thug kumpandisha mtoto wa miaka 14 kwenye stage.

Fahamu kuwa baadhi ya wasanii nchini Marekani wameshatangaza nia ya kugombea Urais nchini humo akiwemo rapper Kanye West ambaye ameonekana kuwa karibu na Rais Trump na kuunga mkono kauli mbiu yake ya ‘Make America Great Again(MAGA)”

VIDEO: WEMA SEPETU AACHIWA HURU, MWANASHERIA ATHIBITISHA

Soma na hizi

Tupia Comments