Viongozi wanne wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP) wakiongozwa na Msemaji wa Mtandao huo Helen Sisya, leo March 14, 2018 wameitika wito baada ya kutakiwa kufika kwa Mpelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kuhusu suala la kupotea kwa Mwenyekiti wao Abdul Nondo ambaye baadaye Jeshi la Polisi lilieleza kuwa hakupotea bali alikwenda kwa mpenzi wake Iringa.
Viongozi hao walifika kwa DCI na kufanya mahojiano wakiwa kama mashahidi kwa takribani zaidi ya saa 8 ambapo baada ya kutoka msemaji wao ameeleza kuwa wametoa ushirikiano huo kwa kuamini kuwa ni suala la kisheria.
Hata hivyo Wakili wao Regnald Martin amezungumza na Ayo TV kwa njia ya simu amesema kuwa alitolewa kwenye mahojiano hayo kwa kile kilichoelezwa kuwa uwepo wake unaweza kuvuruga suala la uchunguzi hivyo hali ni shwari hamna lolote baya mpaka sasa.
Viongozi hao pia ndio waliokuwepo kwenye mkutano na waandishi wa habari siku moja baada ya Nondo kuelezwa kuwa amepotea kwenye mazingira yakutatanisha kabla ya Polisi kukanusha madai hayo.
BREAKING: “Tuzaliane, tufanye kazi la sivyo tutalia tu vyuma vinatubana” JPM