Mix

Pale ambapo kiazi kinatumika kama njia ya kupanga uzazi wa mpango..

on

seed-potato-planting-s4x3_lgKumekuwa na njia mbalimbali za uzazi wa mpango ambazo zinatambulika na kushauriwa kitaalamu, msichana mmoja Colombia amewashangaza madaktari kutokana na njia ambayo ameitumia kwa ajili ya uzazi wa mpango.

Msichana huyo alisema alishauriwa na mama yake kuweka kiazi sehemu zake za siri kama njia ya uzazi wa mpango kuzuia asipate ujauzito.

Binti huyo amesema mama yake ndiye aliyemuonesha njia hiyo ya asili kwa maelezo kwamba kiazi kinapoingizwa sehemu za siri ni njia nzuri ya uzazi wa mpango.

Baada ya kupita wiki mbili alianza kulalamikia maumivu yasiyokuwa ya kawaida na kuamua kwenda clinic, baada ya kufanyiwa uchunguzi aligundulika mizizi inayochipua ikichungulia kutoka kwenye sehemu zake za siri, lakini kiazi hicho kiliondolewa bila kupata athari zozote katika njia yake ya uzazi.

Njia zisizo sahihi na hatari za uzazi wa mpango bado zinaendelea kutumika ulimwenguni kote hasa na mabinti wadogo wanaojihusisha na uhusiano wa kimapenzi kabla ya wakati.

Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments