Klabu ya Napoli imesema “hawakuwa na nia ya kumuudhi au kumkejeli” Victor Osimhen katika chapisho la mtandao wa kijamii lakini hawakumuomba msamaha hadharani.
Klabu hiyo ilishirikisha umma video kwenye akaunti yao ya TikTok ya Osimhen wa Nigeria akikosa penalti, iliyopewa jina la sauti ya juu ikisema ”Nipatie penati tafadhali”-“gimme penalty please”.
Wakala wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ametishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya klabu hiyo.
Taarifa ya Napoli ilisema “kamwe haikuwa nia ya klabu kumkasirisha Victor” ikiwa “iwapo ameona hivyo”.
Chapisho la mitandao ya kijamii limefutwa.
Napoli inaeleza kuwa haikuwahi kumuudhi au kumkejeli Victor Osimhen, ambaye ni kiungo muhimu wa kiufundi wa klabu ,” ilisema taarifa kwenye tovuti ya klabu hiyo.
“Ushahidi wa hili ni ukweli kwamba klabu ilikataa kwa dhati ofa zote ilizopokea za uhamisho wa mshambuliaji nje ya nchi.”
Mkufunzi wa Napoli Rudi Garciaalisema Osimhen ”amewekeza 100%katika klabu hiyo ya Serie A baada ya kufunga bao katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Udinese Jumatano – mechi ya kwanza tangu tukio hilo.
Osimhen aliifungia timu yake bao la pili katika ushindi mnono lakini hakujaribu kushangilia kabla ya kuwindwa na wachezaji wenzake.