Michezo

Rasmi Arturo Vidal amejiunga na timu hii….

on

Vidal1

Baada ya kuwa na uvumi kwa muda mrefu kuhusiana na mchezaji wa kimataifa wa Chile Arturo Vidal anaekipiga katika klabu ya Juventus ya Italia kuhama, July 28 imekuwa ni mwisho wa uvumi huo. Vidal ambaye amekuwa akitakiwa na vilabu kadhaa barani Ulaya ikiwemo Manchester United, amemaliza uvumi huo.

Arturo_Vidal_(Juventus)

Vidal amesaini July 28 katika klabu ya FC Bayern Munich kwa mkataba wa miaka minne hii ikiwa ni ishara ya kumaliza uvumi wa mchezaji huyo kuwa angecheza wapi msimu ujao…. Vidal amesaini mkataba huo mara baada ya kufanyiwa vipimo vya afya asubuhi ya July 28.

vidal

Mkataba huo utamuweka klabuni hapo hadi mwaka 2019. Bayern ilikuwa inahitaji huduma ya Vidal toka mwaka 2011 akiwa katika klabu ya Bayer Leverkusen na baadae kutimkia Juventus ya Italia. Vidal amesajiliwa kwa dau linaltajwa kufikia pound million 28.

Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

 

 

Tupia Comments