AyoTV

VIDEO: Aishi Manula baada ya kurejea Dar, vipi majeraha yake?

on

Timu ya taifa ya Tanzania bara maarufu kwa jina la Kilimanjaro Stars leo imewasili Dar es Salaam ikitokea Kampala Uganda ilipokuwa inashiriki michuano ya CECAFA Senior Challenge Cup 2019 lakini kwa bahati mbaya haikufanya vizuri sana na imeishia nafasi ya nne.
.
Baada ya kurejea Tanzania AyoTV ilimdaka Airport DSM Aishi Manula ambaye alikuwa ni nahodha wa kikosi hiko, anazungumzia kwa Tanzania kuishia nafasi ya nne lakini vipi kuhusu majeraha yake aliyoyapata katika michuano hiyo.
.
Tanzania bara kama utakuwa unakumbuka vizuri ilitolewa katika michuano ya CECAFA hatua ya nusu fainali kwa kufungwa na Uganda wenyeji kwa goli 1-0 lililofungwa na Fahad Bayo dakika ya 85, mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu ikapoteza tena kwa kufungwa na Kenya.

AUDIO: BREAKING: NIYONZIMA KARUDI YANGA SC

Soma na hizi

Tupia Comments