Mchambuzi wa masuala ya soka na mchezaji wa zamani wa timu za Yanga na CDA Dodoma Ally Mayay Tembele ametoa tathmini yake kuhusiana na michuano ya Mapinduzi Cup 2020 inayoendelea visiwani Zanzibar hususa mchezo wa fainali utakaozikutanisha timu za Simba na Mtibwa Sugar.
Mayay ameeleza kuwa mchezo wa fainali mara nyingi huwa hautabiriki kutokana na mchezo huo kuwa hauna utamaduni wa kutegemea matokeo ya mechi zilizopita, hivyo licha ya Simba SC kuonekana kuwa na kikosi bora ila haina maana kuwa wanaweza kupata matokeo kirahisi mbele ya Mtibwa Sugar kama wengi wanavyotarajia.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Mtibwa Sugar na Simba SC ziliingia fainali baada ya Simba SC kuitoa Azam FC kwa mikwaju ya penati 3-2, baada ya game yao dakika 90 kuisha 0-0 wakati Mtibwa wao waliingia fainali kwa kuifunga Yanga SC kwa penati 4-2 hiyo ni baada ya dakika 90 zao kumalizika kwa kufungana 1-1, mchezo wao wa fainali utachezwa January 13 uwanja wa Amaan.
VIDEO: GSM WAMEKULETEA ANTA SPORTS, VIFAA VYOTE VYA MICHEZO ORIGINAL VINAPATIKANA