AyoTV

VIDEO: Baada ya Ligue 1, Ligi Kuu Kenya kufutwa Niyonzima ana ushauri huu VPL

on

Leo Ligi Kuu ya Ufaransa imeitangaza rasmi club ya PSG kama Mabingwa wa Ligi Kuu nchini humo (Ligue 1) kwa msimu 2019/20, hii ni baada ya siku chache zilizopita serikali ya nchi hiyo kutangaza kuwa imesimamisha shughuli zote za michezo nchini humo hadi September 2020, shirikisho la soka Ufaransa likaitangaza PSG kama Mabingwa kwa kuzingatia msimamo ulivyokuwa.

Kenya pia shirikisho la soka nchini humo FKF limeitangaza club ya Gor Mahia kama Bingwa wa Ligi hiyo msimu ukiwa haujamalizika sababu ya corona, kwa upande wa Ligi Kuu soka Tanzania bara mambo bado michezo imesimamishwa kwa muda usiojulikana kwa sababu ya janga la corona.

AyoTV imeongea katika exclusive interview kiungo wa Yanga SC raia wa Rwanda Haruna Niyonzima ana mtazamo gani kuhusiana na hilo Ligi Kuu Tanzania bara vipi iahirishwe tu? tusubiri corona iishe? au Simba SC apewe Ubingwa kwakuwa anaongoza Ligi kwa tofauti kubwa ya point? BONYEZA PLAY KUTAZAMA

AUDIO: MIAKA 38 KITANDANI, MKE WA STAA WA SOKA HAJAKATA TAMAA NA MUMEWE

Soma na hizi

Tupia Comments