Habari za Mastaa

VIDEO: Bella akifunguka kuhusu mjengo wake ‘Wanasema M-Congo namilikije aridhi’

on

Mwimbaji Christian Bella Obama kafunguka kuhusu mjengo wake wa Gorofa alioupost hivi karibuni ambapo kasema tayari kashahamia na anapambana kumalizia Gorofa yake nyingine iliyopo jirani na anapoishi huko Mbweni.

Bella amesema imemchukua miaka 10 kujenga nyumba hiyo ambayo inathamani kubwa na tayari  ameshawanunulia nyumba ya thamani wazazi wake huko kwao Congo tena sehemu ya ushuani.

Pia Bella amegusia ishu ya baadhi ya watu ambao wamekuwa wakihoji  yeye imekuaje amejenga hapa na siyo kwao Congo..? ambapo amesema yeye amezaa na mtanzania na familia yake wanaishi swiden ila watoto wake ni watanzania hivyo hajaona ubaya kujenga nyumba mbili hapa

>>>“Nina Gorofa mbili zote ziko Mbweni, waliniuliza Kwanini najenga hapa wakati nimezaliwa DRC, Nimeanza kufanya kazi huku zamani Nina miaka 15 hapa Tanzania na nimeanza muziki wa Hela tangu 2006, siyo mtu wa attention kwamba nikinunua vitu naanza kutangaza,

”Na ndipo ninapokaa sasa hivi Nishahamia napambania Gorofa yangu ya Pili iishe, Nimezaa hapa Tanzania, wananiulza nimenunuaje hapa hawajui kupitia mtoto wangu naweza kununua, wanauliza vipi na Uraia, Nina miaka 15 nishapiga Hadi show Ikulu” – Bella.

Kutazama Kwa Urefu akifunguka Bonyeza Play video hapa chini…

Soma na hizi

Tupia Comments