Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko amewataka Wafanyakazi kwenye ofisi mbalimbali kuwaheshimu Maboss zao hata kama wanajiona wamewazidi akili na kuepuka kutaka kuwaonesha Watu kuwa Boss ndiye ana matatizo kila panapotokea changamoto.
Dkt. Doto Biteko amesema hayo wakati akiongea na Menejimenti ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake Jijini Dar es salaam “Siri moja muheshimu aliye juu yako hata kama unajiona unamzidi akili muheshimu na yeye aridhike, usitake kuonesha huyu anajua kukosea wewe ndio unajua kupatia utakosea kwa muda mfupi sana”
“Na nakuambia baada ya muda hata huyo unayemuambia siku akiwa anataka kutafuta Mtu wa kumsaidia hatokuchukua wewe kwasababu wewe kule kwetu tunakuita ni Kalomonchocho, Kalomonchocho yupo bize kuhangaika na Boss wake anafanya nini, sio sahihi”
“Sasa wewe una Watu kadhaa unawasimamia hapo chini pengine ni sita, wewe ni Meneja una Watu chini yako 8, 10, 11 kila wakati kukitokea changamoto , unataka kuwaonesha Boss pale juu ana matatizo Mimi sina tatizo hii haitusaidii”